Copenhagen,Denmark.
Zlatan Ibrahimovic usiku wa kuamkia leo ameibuka shujaa baada ya kuifungia Sweden mabao mawili katika mchezo ulioisha kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Denmark katika mchezo mkali wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Ulaya (Euro 2016).
Ibrahimovic aalianza kuipa furaha Sweden dakika ya 19 baada ya kufunga bao kwa kichwa safi akiunganisha kona iliyopigwa na kiungo Kim Kallstrom.Dakika ya 79 Ibrahimovic aliifungia tena Sweden bao la pili kwa mkwaju wa faulo ambao ulikwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa Kasper Schmeichel akichupa bila mafanikio.Mabao ya Denmark yamefungwa na Yussuf Poulsen na Jannik Vestergaard.
Kufuatia ushindi huo Sweden inakuwa imefanikiwa kufuzu kushiriki michuano ijayo ya Ulaya (Euro 2016) itakayopigwa huko Ufaransa kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza.
Baada ya mchezo huo kwisha kama kawaida yake Ibrahimovic hakukosa kitu cha kuongea,amesema "Denmark walisema watatung'oa na kunistaafisha,sasa mimi nimeistaafisha nchi nzima ya Denmark"
0 comments:
Post a Comment