728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, November 22, 2015

    ETOILE DU SAHEL YAIBANA ORLANDO UGENINI,YAJIWEKA KATIKA NAFASI NZURI YA KUTWAA KOMBE LA SHIRIKISHO

    Johannesburg, Afrika Kusini.

    Etoile du Sahel ya Tunisia imejiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa kombe la shirikisho barani Afrika (CAF Confederation) baada ya kuibana Orlando Pirates na kutoka nayo sare ya goli 1-1 katika mchezo wa kwanza wa fainali uliopigwa katika dimba la Orlando,huko Soweto.

    Ammar Jemal aliifungia Sahel goli dakika ya 87 na kuzima shangwe za mashabiki wapatao 30,000 wa Orlando waliokuwa na matumaini ya kushinda mchezo huo baada ya kuwa mbele kwa muda mrefu kwa goli la Thamsanqa Gabuza la dakika ya 36.

    Mchezo wa marudiano utachezwa Novemba 29 huko Tunisia katika dimba la Stade Olympique, Sousse lenye uwezo wa kuchukua watazamaji 25,000.

    Sahel inahitaji ushindi wowote ama sare ya bila kufungana ili iweze kutwaa ubingwa huo wa pili kwa ukubwa barani Afrika.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ETOILE DU SAHEL YAIBANA ORLANDO UGENINI,YAJIWEKA KATIKA NAFASI NZURI YA KUTWAA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top