London,England.
Klabu ya Arsenal imeingia katika mzozo baada ya wanaharakati wa masuala ya mazingira kudai hatua ya klabu hiyo kusafiri kwa ndege kwenda kuivaa Norwich City ni upuuzi na ni uharibufu mkubwa wa mazingira.
Arsenal ambayo leo inavaana na Norwich City saa 19:15 usiku imepondwa na wanaharakati hao kwa madai kuwa hawaoni ni kwanini imeamua kutumia ndege katika safari ya dakika 14 tu wakati ingeweza kusafiri kwa treni na kupunguza uchafuzi wa anga kwa kuwa safari hiyo ni fupi sana.
Wamesema "Kutoka uwanja wa ndege wa London Luton mpaka hapa Norwich International airport ni mwendo wa dakika 14 mpaka 20 lakini Arsenal wameamua kuchukua ndege kwa safari fupi kiasi hiki ya maili 118 badala yake wangetumia usafiri wa treni ili kunusuru uharibifu wa mazingira kwani ingewachukua masaa mawili na nusu pekee kufika Carrow Road"
Hata hivyo, Kocha Mkuu,
Arsene Wenger amesema
wasingeweza kusafiri kwa
basi kwa kuwa wangekutana
na vizuizi vingi vya
barabara kwa kuwa iko
katika matengenezo.
Wenger anaamini usafiri wa
basi, ungechangia uchovu
kwa wachezaji wake hivyo
ndege licha ya kuwa ni
sehemu fupi kwa maana ya
umbali, ndiyo ulikuwa
usafiri sahihi.
0 comments:
Post a Comment