Paris,Ufaransa.
Cristiano Ronaldo huenda akaweka historia ya kuwa mwanasoka wa kwanza kulipwa mshahara wa £500 milioni kwa wiki ikiwa atakubali kujiunga na PSG mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa kutoka nchini Ufaransa zinasema kuwa PSG imemtengea Ronaldo,30 ofa ya £250,000 kama mshahara wake wa wiki hii ni baada ya kukatwa kodi.[Sawa na £500,000 kabla ya kukatwa kodi] ili kuzima ndoto za nyota huyo Mreno kurejea katika klabu yake ya zamani ya Manchester United.
PSG kupitia kwa Rais wake Nasser Al-Khelaifi inamuona Ronaldo kama mrithi sahihi wa nyota wake Zlatan Ibrahimovic ambaye anatarajiwa kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu pindi mkataba wake utakapikuwa umefikia tamati.
0 comments:
Post a Comment