Manchester,England.
Manchester City imeripotiwa kukubali kumsajili kwa mkopo wa miezi mitatu kiungo mkongwe Andrea Pirlo anayekipiga na New York City FC inayoshiriki ligi ya Marekani (MLS).
Kwa mujibu wa Fabio
Caressa wa gazeti la michezo la Italia la "Sky Italia" habari zinasema tayari dili hilo limeshakamilika na Pirlo,36 atajiunga na Manchester City mwezi januari pindi dirisha la usajili litakapokuwa limefunguliwa kutokana na kuwa wakati huo ligi ya Marekani itakuwa mapumzikoni.
Pirlo anakuwa mchezaji wa pili wa New York City FC kujiunga na Manchester City baada ya Frank Lampard kufanya hivyo msimu mmoja uliopita.
0 comments:
Post a Comment