KLABU ya Stand United imeamua kukaa ‘kimya’ kuhusiana na dili la straika wao, Elias Maguli, anayehusishwa kujiunga na Yanga wakati wa dirisha dogo la usajili.
Imeelezwa kwamba Yanga wameanza mchakato wa kumsajili straika huyo aliyeonyesha kiwango cha hali ya juu akiwa na kikosi cha Taifa Stars katika pambano la mtoano kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Algeria katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiwango cha Maguli kinaonekana kumvutia kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm ambaye anataka kuimarisha kikosi chake kwenye mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na michuano ya kimataifa.
Lakini wakati Yanga wakiwa wamepania kumsajili straika huyo wa zamani
wa Simba, uongozi wa Stand United unaonekana kushikwa na kigugumizi kutaja thamani ya staa huyo ambaye ni bidhaa adimu kwenye soko la usajili la Tanzania.
wa Simba, uongozi wa Stand United unaonekana kushikwa na kigugumizi kutaja thamani ya staa huyo ambaye ni bidhaa adimu kwenye soko la usajili la Tanzania.
Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Habari wa Stand, Deo Kija, alisema kwa sasa hawezi kuweka hadharani thamani ya straika wao kwa sababu mambo yaliyo kwenye mkataba ni siri kati ya klabu na mchezaji, hivyo hawawezi kuweka wazi thamani yake kwa sasa.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya Yanga zilieleza kwamba klabu hiyo imemtengea Maguli Sh milioni 40 ili atue Jangwani kwa ajili ya kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
(CHANZO:BINGWA NOV 17)
0 comments:
Post a Comment