Manchester,England.
Ovyo kabisa!!Paul Scholes ameendelea kuikandia klabu yake ya zamani ya Manchester United baada ya kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa jana jumatano wa ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya PSVEindhoven na kutoka sare ya 0-0.
Scholes,41 ambaye kwasasa anafanya kazi BT Sports kama mchambuzi wa soka ameiponda Manchester United na kudai timu hiyo iko mbali sana kuvifika vilabu ya FC Barcelona ama Bayern Munich ambavyo vina safu kali sana ya ushambuliaji.
Amesema "Ovyo kabisa.Huwezi kushindana na kuota kufika mbali katika ligi ya mabingwa kama una safu butu kama hii,Mfano Martial.Haonekani kujali anapokosa magoli,hajali anapofunga goli.Kama mshambuliaji unachopaswa wewe ni kufunga tu hakuna kingine ni kufunga magoli.Haonyeshi kama ni aina ya wale washambuliaji tunaowajua,nadhani Manchester United wanapaswa kuingia tena sokoni mwezi januari kusaka mshambuliaji mwingine.Manchester United haionyeshi kama ina njaa ya kufunga magoli"
Scholes ameongeza "Sikuona hatari yoyote langoni kwa PSV toka washambuliaji wetu,hata kama utakuwa vizuri kisai gani katika kujilinda lakini kama hauna washambuliaji wa kufanya maajabu kidogo langoni kwa wapinzani bado utahangaika tu.Ukivitazama vilabu vingine kama Barcelona ama Bayern Munich washambuliaji ndio wanaoleta tofauti uwanjani siyo viungo wala walinzi.
Martial amejikuta akikosolewa na Scholes baada ya kushindwa kufunga mara mbili katika kipindi cha kwanza licha ya kuwa katika nafasi nzuri.

0 comments:
Post a Comment