728x90 AdSpace

Saturday, November 21, 2015

DORTMUND YAKIONA CHA MOTO YADUNDWA 3-1 NA HAMBURG, AUBAMENYANG YEYE AZIDI KUTUPIA TU

Hamburg,Ujerumani.

Borussia Dortmund imekiona cha moto usiku wa kuamkia leo baada ya kukutana na kipigo cha magoli 3-1 toka kwa Hamburg SV katika mchezo mkali wa ligi ya Bundesliga uliopigwa katika dimba la Volksparkstadion.

Borussian Dortmund ambayo ilikuwa haijashinda mchezo wowote nyumbani kwa Hamburg kwa kipindi cha misimu minne ilijikuta ikiendeleza rekodi hiyo baada ya kuruhusu magoli ya Pierre Michel Lasogga (19./pen),Lewis Holtby (41.) na goli la kujifunga la mlinzi wake Hummels (55.) huku goli lake la kufutia machozi likifungwa na Pierre Emerik Aubameyang (85).

Kufuatia kichapo hicho Borussian Dortmund imebaki nafasi ya pili ikiwa nyuma ya Bayern Munich kwa tofauti ya pointi tano.Tofauti hiyo inaweza kuongezeka ikiwa Bayern itaifunga Shalke 04 katika mchezo utakaopigwa leo jioni.

VIKOSI

HSV: Adler - G. Sakai, Spahic (29. Cleber), Djourou, Ostrzolek - Kacar (73. Gregoritsch) - Jung, Holtby (82. Diaz) - Müller, Ilicevic - Lasogga

Borussia Dortmund: Bürki - Ginter (46. Piszczek), Sokratis, Hummels, Schmelzer - Weigl, Gündogan - Reus (69. Januzaj), Kagawa (46. Castro), Mkhitaryan - Aubameyang


Lasonga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: DORTMUND YAKIONA CHA MOTO YADUNDWA 3-1 NA HAMBURG, AUBAMENYANG YEYE AZIDI KUTUPIA TU Rating: 5 Reviewed By: Unknown