Fainali za kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, zinazojulikana kama CECAFA Senior Challenge Cup, zinatazamiwa kuanza leo jumamosi Novemba 21 hadi Disemba 6, nchini Ethiopia.
Nchi 11 zitashiriki michuano hiyo, huku Malawi ikishiriki kama timu mwalikwa.
Katika michuano ya ufunguzi Jumamosi ya Novemba 21, mwenyeji Ethiopia itachuana na Rwanda katika mji mkuu Addis Ababa, wakati vijana wa Burundi watakuwa wanatoana jasho na mahasimu wao kutoka visiwa vya Zanzibar. Bingwa mara 13 wa mashindano hayo Uganda Cranes watafungua kampeni zao dhidi bingwa mtetezi wa taji hilo Kenya siku ya Jumapili, Novemba 22. Kenya ilitwaa taji hilo la Kombe ya Kagame mwaka wa 2013, baada ya kuisasambua Sudan mabao 2-0 katika fainali, ambapo vijana wa Harambee Stars walikuwa wanaupiga nyumbani jijini Nairobi.
Mashindano hayo hayakufanyika mwaka jana wa 2014 kwani Uhabeshi walisema hawana fedha za kuyaandaa. Rwanda iliteuliwa kuandaa michuano ya mwaka huu iwapo Ethiopia ingefeli tena.
Licha ya machafuko kuendelea kushuhudiwa Somalia, nchi hiyo ya Pembe ya Afrika itatuma timu ya kuiwakilisha kwenye michuano hiyo. Somalia itatoana udhia na Tanzania katika mchuano wao wa ufunguzi mnamo Novemba 22.
Nchi zingine zitakazoshiriki mashindano hayo ya kieneo ni Eritrea, Djibouti, Sudan na Ethiopia.
MAKUNDI
KUNDI A
1. Ethiopia
2. Tanzania bara
3. Zambia
4. Somalia
KUNDI B
1. Burundi
2. Djibouti
3. Kenya
4. Uganda
KUNDI C
1. Rwanda
2. Sudan
3. Sudan Kusini
0 comments:
Post a Comment