728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, November 21, 2015

    MAN UNITED YAITUNGUA WATFORD 2-1,YAONGOZA LIGI KWA MUDA,DEPAY SAFI,HERRERA AUMIA

    Watford,England.

    Manchester United imekalia kwa muda kiti cha uongozi wa ligi kuu England baada ya leo mchana kuilaza Watford kwa bao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa huko Vicarage Road.

    Magoli yaliyoipa ushindi Manchester United yamefungwa na Memphis Depay dakika ya 11 akimalizia vyema pasi ya kiungo Ander Herrera ambaye dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza alilazimika kutoka baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Marcos Rojo huku lile la pili likipatikana dakika ya 90 baada ya Troy Deeney kujifunga akiwa katika harakati za kuokoa kabla ya hapo nyota huyo alikuwa ameifungia goli Watford dakika ya 87.

    Kufuatia ushindi huo Manchester United imefikisha pointi 27 na kuongoza ligi ikiviacha katika nafasi ya pili na tatu vilabu vya Manchester City na Arsenal ambavyo vitashuka dimbani muda mfupi ujao.Vyote vina pointi 26.

    Vikosi

    Manchester United: De Gea; Young,Jones, Smalling, Blind; Schneiderlin,Schweinsteiger; Mata, Herrera/Rojo,Lingard,Memphis. 

    Watford: Gomes; Nyom, Cathcart,Britos, Anya; Capoue, Watson; Abdi,
    Jurado, Deeney; Ighalo. Subs:
    Arlauskis, Oularé, Paredes, Aké,Guedioura, Ibarbo,Diamanti.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN UNITED YAITUNGUA WATFORD 2-1,YAONGOZA LIGI KWA MUDA,DEPAY SAFI,HERRERA AUMIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top