728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, November 26, 2015

    ISCO ATUPWA JELA YA SOKA

    Madrid,Hispania.


    Nyota wa Real Madrid Isco anatarajiwa kuwa nje ya dimba kwa majuma mawili baada ya kufungiwa kutokana na kosa la kumpiga teke la makusudi nyota wa FC Barcelona Neymar Jr.


    Isco,23 aliyeingia dimbani kipindi cha pili katika mchezo wa El Clasico alijikuta akitolewa nje  kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi David Fernandez Borbalan kwa kosa la kumpiga teke kwa makusudi Neymar Jr tena bila ya kuwa hata na mpira.

    Kufuatia hukumu hiyo Isco ataukosa mchezo wa jumapili hii ugenini dhidi ya Eibar (Novemba 29) kisha siku saba baadae dhidi ya Getafe (Desemba 5)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ISCO ATUPWA JELA YA SOKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top