728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, November 16, 2015

    BAO LAKAMILISHA USAJILI WA MAGULI YANGA


    BAO la mshambuliaji Elius Maguli wakati akiitumikia timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, limeonekana kuchagiza mchakato wa Klabu ya Yanga kukamilisha usajili wa nyota huyo kwa mabingwa hao wa soka nchini.
    Maguli alifunga bao nzuri juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakati Taifa Stars ilipocheza na Algeria katika mchezo wa kutafuta kupangwa katika makundi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
    Licha ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, lakini makocha wa Yanga, Hans van der Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi, waliokuwapo uwanjani hapo wakilazimika kufanya kazi ya ziada kumjadili mshambuliaji huyo.
    Pluijm alionekana kuvutiwa na Maguli jinsi alivyocheza na hata alipofunga bao hilo kiufundi kwa kichwa dakika ya 42. Pluijm alishindwa kuvumilia na badala yake alimwita msaidizi wake Mwambusi na kujadili kwa dakika kadhaa.
    Mwambusi anaelezwa kulipendekeza jina la Maguli katika ripoti yake kutokana na kazi maalumu aliyopewa na Pluijm ya kuangalia mikanda ya timu zote zilizocheza katika Ligi Kuu kabla haijasimama.
    (CHANZO:BINGWA)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAO LAKAMILISHA USAJILI WA MAGULI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top