Olunga
Awassa,Ethiopia.
Michuano ya Cecafa Chalenji Cup imeendelea tena leo kwa mechi mbili kupigwa huko Awassa,Ethiopia.
Katika mchezo wa kundi B Kenya na Burundi zimegawana pointi baada ya kutoka sare ya goli 1-1.Goli la Burundi limefungwa na Hamis Tambe dakika ya 11 baada ya kazi nzuri ya Fwadi Ndasiyenga huku Kenya ikisawazisha dakika ya 41 kupitia kwa Michael Olunga akimalizia kazi nzuri ya Clifton Miheso na Jacob Keli.
Kufuatia matokeo hayo Kenya na Burundi vimefikisha pointi nne na kuendelea kuongoza kundi B zikifuatiwa na Uganda yenye pointi nne na mkiani iko Zanzibar Heroes ambayo mpaka sasa haina pointi yoyote.
Katika mchezo wa kundi C,Malawi imeendeleza ubabe baada ya kuifunga Djibout kwa magoli 3-0.
Magoli ya Malawi yamefungwa na Gerlad Phiri Jnr,John Banda na Chiukepo Msowoya.
0 comments:
Post a Comment