London,England.
Chelsea imeibana Tottenham na kutoka nayo sare ya bila kufungana katika mchezo mkali wa ligi kuu uliopigwa mchana wa leo katika dimba la White Hart Lane,London.
Katika mchezo huo ulitazamiwa na wengi kuwa ungekuwa mgumu na wa kuvutiwa ulishuhudia dakika zote tisini zikiisha bila ya wavu wowote kutikiswa licha ya vilabu vyote kupata nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa Son Heung-min na Pedro Rodriguez.
Kufuatia matokeo hayo Chelsea imepanda kwa nafasi moja toka nafasi ya 15 mpaka ya 14 baada ya kujikusanyia pointi 15 katika michezo 14,Tottenham wao wako nafasi ya 5 baada ya kujikusanyia pointi 25.
Diego Costa achafua hali ya hewa ugenini.
Diego Costa ameendelea kuonyesha kuwa yeye ni mtukutu kupindukia kufuatia kugoma kufanya mazoezi (warm up) na wachezaji wenzake baada ya kuambiwa hayumo katika kikosi cha kwanza ambacho kilianza mchezo leo hii.
Vikosi
TOTTENHAM XI (4-2-3-1): Lloris; Walker,Alderweireld,Vertonghen,Rose,Mason (Lamela), Dier, Dembele,Son, (Njie); Eriksen; Kane.
CHELSEA XI (4-2-3-1): Begovic,Ivanovic, Zouma, Cahill, Azpilicueta,
Fabregas,Matic,Willian 6 (Kennedy), Oscar, Pedro 6 (Loftus-Cheek);Hazard
0 comments:
Post a Comment