Chirwa na Ngoma.
Dar es Salaam,Tanzania.
MSHAMBULIAJI Obrey Chirwa muda wowote atatangazwa kukamilisha uhamisho kujiunga na wababe wa soka la Tanzania,Young African Sports Club (Yanga).
Raia huyo wa Zambia anataraji kuwasili Tanzania leo kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga huku ikisemekana Yanga wamelazimika kulipa zaidi ya $100 000 kupata sahihi ya Chirwa.
Yanga wana matumaini makubwa kuwa Chirwa atafanya vizuri kama walivyofanikiwa wachezaji wenzie wa zamani wa FC Platinum Donald Ngoma na Thabani Kamusoko.
Mwaka jana Chirwa aliachana na Horbo IK ya Denmark baada ya kutovutiwa na maslahi katika klabu hiyo kisha akaamua kurudi timu yake ya awali FC Platinum.
0 comments:
Post a Comment