Toulouse,Ufaransa.
ITALIA imefuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Ulaya/Euro 2016 baada ya jioni ya leo kuifunga Sweden kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa Kundi E uliocheza katika uwanja wa Stade de Toulouse ulioko katika mji wa Toulouse.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Elder Martins dakika ya 88 kwa mkwaju mkali wa karibu baada ya kupokea pasi ya kichwa toka kwa Simone Zaza.
Kwa matokeo hayo Italia imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya 16 bora baada ya kufikisha pointi sita kufuatia kushuka dimbani mara mbili.
VIKOSI
Sweden : Isaksson; Johansson, Lindelof, Granqvist,Olsson; Larsson, Ekdal, Kallstrom, Forsberg;Guidetti, Ibrahimovic
Italy : Buffon; Barzagli, Bonucci, Chiellini;Florenzi, Candreva, Parolo, De Rossi,Giaccherini; Eder, Pelle
0 comments:
Post a Comment