728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 17, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA IJUMAA YA LEO JUNI 17,2016.

    N'Golo Kante

    Kante:Mbio za kuiwania saini ya kiunga mahiri wa Leicester City, Mfaransa N'Golo Kante,25, zimezidi kunoga baada ya Real Madrid nayo kuripotiwa kuitaka huduma ya kiungo huyo wa zamani wa Caen mwenye thamani ya £20m.(El Confidencial)

    Azpilicueta:Meneja wa Manchester United Mreno Jose Mourinho anataka kuitikisa klabu yake ya zamani ya Chelsea kwa kutuma ofa ya kumsajili mlinzi wa kulia wa klabu hiyo Muhispania Cesar Azpilicueta,26,anayewindwa pia na vilabu vya Paris Saint-Germain na Athletic Bilbao.(AS )

    Dembele :Arsenal imeungana na Chelsea katika mbio za kuiwania saini ya mshambuliaji aliyegomea mkataba mpya Fulham,Mfaransa Moussa Dembele.Msimu uliopita Dembele,22,aliifungia Fulham mabao 15 na kutengeneza mengine sita katika michezo 43.Mwezi ujao Dembele ataondoka Fulham akiwa mchezaji huru baada ya kugomea mkataba moya Craven Cottage.(ESPN)

    Hyndman:Bournemouth imefanikiwa kumsajili mlinzi wa Fulham Emerson Hyndman.Hyndman,20,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuichezea Bournemouth baada ya kumaliza mkataba Fulham.(Sky Sports)

    Balde:Real Madrid imefikia makubaliano ya kumsajili winga wa AS Lazio,Msenegal Keita Balde .Balde,21,aliyeanzia soka lake katika shule ya soka ya La Masia inayomilikiwa na Barcelona atapimwa uwezo na Meneja Zinedine Zidane ili kufahamu kama yuko tayari kubaki kikosi cha kwanza ama atolewe kwa mkopo ili kuongeza makali.(Mundo Deportivo)

    Ounas:Manchester United inajiandaa kutuma ofa ya £9m ili kumsajili winga wa Bordeaux Adam Ounas,20.(RMC)

    Strootman:Everton imeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa AS Roma Mholanzi Kevin Strootman,26.Kutoka England habari zinasema Everton iko tayari kutoa £30m ili kumnasa kiungo huyo aliyecheza michezo 12 pekee msimu uliopita kutokana na kusumbuliwa na majeruhi kwa muda mrefu.(Daily Mail)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA IJUMAA YA LEO JUNI 17,2016. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top