Habari na George James/Paul Manjale
Stone:Kocha Jose Mourinho amethibitisha Chelsea FC itakamilisha usajili wa beki wa Everton ,John Stones ambaye anaonekana kuja kuwa mbadala wa kapteni John Terry, ingawa meneja wa Everton Roberto Martinez amesisitiza mchezaji uyo hauzwi kokote lakin Chelsea FC itaongeza ofa ya Euro 32 kwaajili ya beki uyo
wiki hii.
Gourcuff:Klabu ya Arsenal huenda ikafanya usajili wa kushitukiza kwa kumsajili kiungo Yoann Gourcuff,29 ambaye kwa sasa hana timu baada ya kutemwa na Olympique Lyon.Habari zinasema kocha Arsene Wenger ni shabiki wa kiungo ambaye wakati anachipukia alikuwa ajifananishwa na Zinedine Zidane.(talkSPORT)
Dzeko:Klabu ya Arsenal inafikiria kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Edin Dzeko 29 kwa ajili ya kuleta changamoto kwa mshambuliaji wake Oliver Giroud.Dzeko ameichezea Manchester City michezo 130 na kufunga magoli 50 goals tangu ajiunge nayo mwaka 2011.(Daily Star)
Lewandowski:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuandaa kitita cha £102.4m kwa ajili ya kuwasajili washambuliji wawili wa Bayern Munich Thomas Muller na Robert Lewandowski.(Daily Express)
Berahino:Klabu ya Tottenham mapema wiki ijayo itatuma kitita cha £15m kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino.(Sunday Express)
Verratti:Klabu ya Barcelona kupitia kwa mkurugenzi wake wa michezo Ariedo Braida imeripotiwa kuwa imeanza kufanya mazungumzo ya a wali na klabu ya Paris Saint-Germain kwa ajili ya kumsajili kiungo Marco Verratti,22 katika kipindi ambacho jitihada za kumsajili Paul Pogba zikionekana kugongwa mwamba.(Mundo Deportivo)
Mitrovic:Mshambuliaji wa Anderletch Mserbia Aleksandar Mitrovic kesho jumatatu atafanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea klabu Newcastle United kwa ada ya uhamisho ya £13m.(Sky Sports)
Vidic:Klabu ya Everton imeripotiwa kuwa itamsajili mlinzi wa klabu ya Middlesbrough Ben Gibson ikiwa itashindwa kumsajili mlinzi wa zamani wa Manchester United Nemanja Vidic.(Mirror)
Mirallas:Klabu ya West Ham United imetuma ofa ya £6m kwenda katika klabu ya Everton kwa ajili ya kuitaka saini ya winga Mbelgiji Kevin Mirallas,27.Hata hivyo habari za ndani zinasema Everton haitamuachia nyota huyo kwa dau la chini ya £8m.(The Daily Mirror)
Lacazette:Mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette,24 ameviacha kwenye mataa vilabu vya Arsenal na Liverpool baada ya kusema kuwa hana mpango wa kuihama klabu ya Lyon katika kipindi hiki cha usajili.(Goal)
0 comments:
Post a Comment