Straika wa Nigeria Odion Ighalo amesema tofauti ya viwanja iliyopo kati ya Ulaya na Afrika ndiyo inayofanya afunge mabao mengi zaidi klabuni kuliko katika timu yake ya taifa.
Ighalo anayekipiga Watford inayoshiriki ligi kuu nchini England anaamini ubovu wa viwanja vya soka katika nchi nyingi za Afrika,hali ya hewa na soka la kukamiana ndivyo vimekuwa sababu ya yeye kushindwa kutamba katika kikosi cha Nigeria kama ambavyo anafanya katika kikosi cha Watford.
Akifanya mahojiano na gazeti la New Telegraph,Ighalo amesema
"Hatuwezi kulinganisha vitu vingi vilivyopo Ulaya na vile tulivyonavyo Afrika.Ukiongelea viwanja kati ya Ulaya na Afrika utaona kuwa kuna tofauti kubwa sana kama ilivyo katika upande wa hali ya hewa"
"Jambo jingine ni ugumu wa soka la Afrika,watu wanachezaji kwa nguvu sana na kukamiana lakini kama straika napaswa kupambana na kila hali"Alimaliza Ighalo ambaye ameifungia Watford mabao tisa mpaka sasa huku akifanikiwa kuifungia Nigeria mabao mawili pekee katika michezo saba.
0 comments:
Post a Comment