Athens,Ugiriki.
Arsenal imefuzu hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya usiku wa leo kuibuka na ushindi mnono wa magoli 3-0 dhidi ya Olympiakos katika mchezo mkali wa kundi F uliopigwa huko Georgios Athens,Ugiriki.
Arsenal ambayo iliingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa magoli 3-2 na Olympiakos katika mchezo wa awali uliopigwa katika dimba lake la Emirates imepata magoli yake yote kupitia kwa mshambuliaji Mfaransa Olivier Giroud.
Giroud alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 29 kwa kichwa cha kuchupa akiunganisha krosi ya Aaron Ramsey toka upande wa kushoto kisha akaongeza la pili dakika ya 49 akimalizia kazi nzuri ya Joel Campbell na dakika ya 67 akafunga kazi kwa kufunga goli la tatu kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya mlinzi wa Olympiakos Omar Elabdellaoui kuunawa mpira wa krosi wa mlinzi wa Arsenal Nacho Monreal.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Chelsea nayo imefuzu baada ya kuitandika FC Porto kwa magoli 2-0 katika mchezo wa kundi G uliopigwa Stamford Blidge.Magoli yaliyoipa Chelsea ushindwa yamefungwa na Marcano dakika ya na Willian dakika ya 52.
Matokeo mengine
Valencia 0-2 Lyon
Roma 0-0 Bate
Zagreb 0-2 Bayern Munich
Gent 2-1 Zenit
Bayer Leverkusen 1-1 Barcelona
Dynamo Kiev 1-0 Maccabi Tel Aviv
0 comments:
Post a Comment