Dakar,Senegal.
Timu ya taifa ya Nigeria ya U23 imekuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Olympic ya mwaka 2016 itakayofanyika Rio de Janeiro,Brazil baada ya leo kuibanjua Senegal kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa Dakar,Senegal.
Goli lililoipa Nigeria ushindi limefungwa dakika ya 75 na nahodha Peter Etebo kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Senegal Ousseynou Thioune kuunawa mpira katika eneo la hatari kabla ya hapo Senegal ilishindwa kuongoza baada ya penati ya Ibrahima Sory Keita kudakwa na kipa wa Nigeria Emmanuel Daniel.
Kufuatia matokeo hayo Senegal inahitaji kucheza na timu moja kati ya Algeria ama Afrika Kusini ili kukamiliasha timu tatu zitakazoiwakilisha Afrika katika michuano ya mwakani huko Rio de Janeiro.
0 comments:
Post a Comment