Liberty,Wales.
Swansea City leo imemtimua aliyekuwa kocha wake mkuu Garry Monk kufuatia muendelezo wa matokeo mabovu katika ligi kuu nchini England.
Swansea City kupitia kwa mwenyekiti wake Huw
Jenkins imetangaza kumtimua Monk baada ya kufanikiwa kushinda mchezo mmoja tu kati ya kumi na tatu ya ligi kuu hiki ikiwa pointi moja tu juu ya mstari wa kushuka daraja.
Monk alianza kuifundisha Swansea City Februari 2014 akichukua nafasi ya Michael Laudrup katika mchezo ambao Swansea City iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Cardiff City na kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nane.
Mbali ya Swansea City vilabu vingine vya England ambavyo navyo vimetimua makocha msimu huu ni Liverpool, Aston Villa na Sunderland.
Wakati huohuo makocha Brendan Rodgers na Gus Poyet wametajwa kuwa mstari wa mbele kuchukua mikoba ya Garry Monk katika klabu ya Swansea City.
0 comments:
Post a Comment