728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, December 09, 2015

    JOSEPH KANIKI ABAKISHA MUDA MFUPI ATOKE JELA

    Ethiopia. Mshambuliaji wa zamani wa Simba anayetumikia kifungo cha miaka saba na nusu jela nchini Ethiopia, Joseph
    Kaniki ‘Golota’, huenda akazitazama fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini
    Russia akiwa uraiani.

    Golota alianza kutumikia kifungo cha miaka saba na nusu jela mwaka 2012
    baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya akiwa safarini kwenda
    Ulaya.

    Mshambuliaji huyo alikamatwa sanjari na
    bondia wa Tanzania,Mkwanda Matumla
    wakiwa katika harakati za kuunganisha ndege kwenye Uwanja wa Ndege wa
    Kimataifa wa Addis Ababa.

    Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia anayeshuighulikia Amani na Usalama, Sevike Ndatta,alisema Golota na Mkwanda wamebakiza miaka miwili na nusu ya kutumikia adhabu zao.

    Ndatta alisema kwa hesabu za kifungo,wanamichezo hao wa Tanzania wamebakiza miaka miwili na nusu, hivyo
    katikati ya 2017 watakuwa huru.

    “Kaniki (Golota) na Mkwanda (Matumla) ni miongoni mwa Watanzania sita wanaotumikia kifungo nchini Ethiopia,wakati wengine wawili wakiwa mahabusu,” alisema Ndatta.

    Ofisa huyo aliongeza kwamba Golota anaungana na Watanzania wengine wanane
    katika kesi inayofanana ya kuhusika na usafirishaji wa dawa za kulevya kupitia
    Uwanja wa Ndege wa Addis Ababa.

    “Sheria za usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya ni ngumu katika nchi zote. Tunachofanya kama ubalozi ni kutoa msaada ambao upo ndani ya uwezo wetu,tunafika mara kadhaa kuwaona na
    kuwapa mahitaji,” aliongeza ofisa huyo wa kibalozi.

    Ndatta alisema, mshambuliaji huyo amepewa msaada mkubwa wa kuhakikisha anatoka, lakini bila mafanikio kutokana na ushirikiano mdogo wanaoupata wanapopiga namba za watu
    anaodai ni ndugu zake kusikia kuwa wanazungumza na Serikali.

    Aidha, Ndatta alitoa wito kwa vijana wa Kitanzania wasikubali kujiingiza kwenye
    biashara ya dawa za kulevya kutokana na ukali wa adhabu yake pindi wanapotiwa hatiani.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JOSEPH KANIKI ABAKISHA MUDA MFUPI ATOKE JELA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top