Dar es Salaam. Wakati rungu la Rais John Magufuli kuhusu wakwepa kodi likitua Shirikisho la Soka Tanzania nchini (TFF),klabu za Ligi Kuu zikiwamopamoja na
Simba na Yanga zimeanza kuweweseka juu ya hatma yao kwa suala la kodi za
mishahara ya wachezaji (Paye).
Tayari Mamlaka ya Mmapato
Tanzania (TRA) Manispaa ya Ilala imefungia akaunti za TFF kwa kushindwa kulipa kodi mbalimbali ikiwaemo ile ya Paye inayotokana na
malipo ya mishahara ya makocha wa timu ya Taifa na watendaji wengine wa
Shirikisho hilo.
Ofisa Mwandamizi Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Hamisi Lupenja amesema kuwa hakuna klabu itakayokwepa rungu hilo.
“Hakuna atakayekwepa mkono wa sheria,katika hili kila mmoja atawajibika, kwa
klabu kila moja inapaswa kulipa kulingana na makubaliano wasipofanya
hivyo kwa wakati tuliokubaliana hatua
stahiki zitafuata,” alisema Lupenja.
“TFF ilikuwa ikidaiwa madeni ya nyuma na imeshindwa kuyalipa kwa wakati ndiyo sababu ya akaunti zake kufungwa,mbali na TFF pia tutaangalia na klabu,suala la kodi ni sheria na hakuna yoyote atakayekwepa,”alisema.
0 comments:
Post a Comment