728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 14, 2017

    Nyota wa Leicester City amwacha mke wa ndoa baada ya kuwekewa ngumu kuoa mke wa pili


    Leicester,England.

    NYOTA wa Leicester City,Mnigeria,Ahmed Musa ameachana na aliyekuwa mke wake wa ndoa,Jamila Musa.Hii ni kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa wawili hao.

    Musa,24,ambaye wiki iliyopita alifikishwa kituo cha polisi cha jijini Leceister kwa madai ya kumpiga mkewe huyo baada ya kutokea kutoelewana kati yao ameripotiwa kumwacha mwanamke huyo aliyezaa naye watoto wawili baada ya kuwekewa ngumu kuoa mke wa pili licha ya dini yao ya kiislamu kutoa ruhusa. 

    Musa alitaka kuoa mke wa pili kama inavyoruhusiwa na dini yake ya kiislamu lakini mke wake Jamila alikuwa akipinga jambo hilo.Kwa kipindi kirefu walikuwa na mgogoro kati yao.Amesema rafiki huyo wakati akifanya mahojiano na mtandao wa Owngoalnigeria.com

    Musa alijiunga na Leceister City mwezi Agosti mwaka jana akitokea CSKA Moscow ya Urusi kwa ada ya Pauni Milioni 16.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nyota wa Leicester City amwacha mke wa ndoa baada ya kuwekewa ngumu kuoa mke wa pili Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top