Manchester, England.
JUAN Mata (Pichani) akishangilia bao la pekee la dakika ya 70 aliloifungia Manchester United na kuipeleka robo fainali ya kombe la Europa Ligi katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Rostov jana Alhamis nyumbani Old Trafford.
Mata amefunga bao hilo akimalizia krosi ya Henrikh Mkhitaryan iliyoguswa kidogo na Zlatan Ibrahimovic na kuipa Manchester United ushindi wa jumla wa mabao 2-1 hii ni baada ya kutoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wa awali uliochezwa huko Urusi juma moja lililopita.
BOFYA HAPA KWA MATOKEO ZAIDIhttp://www.bbc.com/sport/football/europa-league/results
0 comments:
Post a Comment