Manchester,England.
KIUNGO wa Manchester United,Paul Pogba atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha wiki mbili mpaka tatu baada ya jana Alhamis kupata jeraha la misuli wakati akiichezea Manchester United kwenye mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora wa michuano ya Europa Ligi dhidi ya FC Rostov uliofanyika dimbani Old Trafford na wenyeji kushinda kwa bao 1-0.
Pogba,24,alilazimika kutolewa uwanjani katika dakika ya 47 ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Marouane Fellaini baada ya kuonyesha kuwa asingeweza kuendelea kuipigania Manchester United mbele ya Warusi,FC Rostov.
Hii ina maana kwamba Pogba ataukosa mchezo wa Jumapili hii wa ligi kuu England dhidi ya Middlesbrough.Pia hatakuwa sehemu ya kikosi cha Ufaransa ambacho baadae mwezi huu kitakuwa na michezo miwili ya kimataifa dhidi ya Luxembourg na Hispania itakayofanyika kwenye dimba la Parc des Princes.
Mbali ya Pogba,Mdachi Daley Blind pia alishindwa kumaliza mchezo dhidi ya FC Rostov na nafasi yake kuchukuliwa na Phil Jones katika dakika ya 64 baada ya kupata jeraha dogo lililotokana na kugongwa kwenye kifundo cha mguu.
0 comments:
Post a Comment