Monaco,Ufaransa.
Nyota wa klabu ya Monaco, Bernardo Silva amekiri kufurahishwa na taarifa zinazomuhusisha na vilabu vya Manchester United na Chelsea lakini anafuraha kubaki ligi kuu ya Ufaransa kwa sasa.
"Ndio nimesikia hizo taarifa. Sina uhakika kama ni za kweli au za uongo. Bila shaka ni faraja sana kuhusishwa na vilabu kama hivyo lakini sijafikiria kuhusu swala hilo ."
"Siku moja nitapenda kucheza Uingereza au Hispania katika moja ya ligi bora Duniani, lakini kwa sasa nina furaha nilipo."
0 comments:
Post a Comment