Kiungo mshambuliaji wa
klabu ya Chelsea Mbrazil Oscar Dos Santoa (22) ameelezea kitu kinachomnyima
usingizi na kumkera klabuni hapo.Akifanya mahojiano na jarida la klabu hiyo
Oscar amesema…
“Huwa nachukia
sana pasi yangu isipomfikia mchezaji mwenzangu wa Chelsea.Mimi ni mtu mshindani
sana na ninapenda kushinda kila mchezo.Nataka pasi zangu zote ziwafikie walengwa
na mara zote napenda kufunga,ndiyo nilivyo”.
“Kama
mechi ni ngumu sitoki naendelea kupambana mpaka kieleweke.Mimi ni mchezaji
mbunifu,mpambanaji napenda kutimiza majukumu yangu uwanjani.Napenda kutengeneza
nafasi na pia kuwa na mpira mguuni.Nisipokuwa na mpira nafanya kila jitihada
ili niupate na kuhakikisha napambana ili kuisaidia timu yangu iibuke na ushindi”
0 comments:
Post a Comment