Nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea Muireland Tony Cascarino anaamini kuwa
mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Muhispania Diego
Costa atakuwa bora zaidi ya gwiji na mchezaji mwenzie raia wa Ivory Coast Didier Costa “Tito”
alyeifungia klabu hiyo jumla ya magoli 157 katika misimu minane akitokea klabu
ya Marseille ya Ufaransa.
Cascarino akiwa na Denis Wise enzi akichezea klabu ya Chelsea |
Baada ya kumshuhudia Diego Costa akifunga magoli saba katika
michezo minne ya Epl,Cascarino anaamini Costa ni bora hata zaidi ya yule Drogba
wa misimu kadhaa iliyopita.
Cascarino amesema “Nafikiri
Costa ni bora kuliko Drogba.Amekuwa akihaha kwenye eneo la adui muda wote bila
kuchoka.Najua ni mapema,lakini nafikiri kuna njaa na hasira ndani yake na kwa
kiasi fulani namuona yuko vizuri kinguvu kuliko Drogba.Lakini anapaswa
kupunguza kidogo hilo na kuendelea na njaa ile ile.Kama anaweza kufanya hilo na kuwa
mbali na majeruhi hakuna shaka ndiye atakayeibuka kuwa mfungaji bora wa Epl
msimu huu.
0 comments:
Post a Comment