MAKALA YA LEO
Allen Kaijage
0655106767
kaijagejr@gmail.com
Thamani ya mtu ipo kwenye umuhimu wa mtu pia
upendo kwa kitu au mtu upo kwenye thamani ya mtu au kitu husika.Sentesi hii si
sheria ingawa imeegemea kwenye ukweli .Ukitaka
kujua ukweli wake angalia watu wanaoheshimiwa kwenye jamii wana umuhimu gani
kwenye hiyo jamii?,pia chunguza vitu
vinavyopendwa na kuheshimiwa duniani vina umuhimu gani kwa watu?.Najua majibu
ya ubongo wako hayatotofautiana sana na fikra zangu.Ila sentesi hii imekuwa
haina mahusiano na bara letu la Afrika
,hasa nchi yetu Tanzania.ukiwa mtanzania lazima utakataakataa kuunga mkono
sentesi hii,Hasa pale uinapoona vitu vyenye thamani havisaminiwi wala kutiliwa
maanani.
Kuna
watu wengi sana ni muhimu kwenye jamii yetu ila hawathaminiwi.pia vipo vingi
vyenye thamani lakini tumevipuuzia.Moja ya watu muhimu tusiowathamini kwenye
jamii yetu ni walimu.Walimu wana hali
ngumu sana hata wagosi wa kaya walishawai kuwaimbia.Ukiangalia watu wote wenye
thamani wamepitia kwenye mikono ya mwalimu,Walimu wamekuwa kama makopo ya
chumvi yainahifadhi chumvi na kufanya chumvi iwe salama mpaka wakati wa kuandaa
chakula.Lakini ukichunguza makopo mengi ya chumvi mara nyingi hayawi kwenye
hali ya usafi.Mpishi bila chumvi hawezi kupika chakula,lakini hasilani hawezi
kukumbuka umuhimu wakifaa kinachohifadhi
chumvi hiyo.
Huku kwenye soka pia tunayo makopo yetu ya chumvi.Makopo hayo ni
kama mengine kuhusu swala la kuthaminiwa.Makocha wengi sana Tanzania
hawathaminiwi,Hivi juzi tu tumetoka kusikia malalamiko ya makocha wazawa.Hakuna
anayewajali ,Ila lengo langu si kuwazungumzia wakina Julio,Msolla,Kayuni na
wengine ambao angalau walishawai kupata nafasi ya kutoa walichonacho.Hapa
nataka niwazungumzie makocha wenye uwezo mkubwa lakini hawathaminiwi kama
makopo ya chumvi ya wapishi wengi.
Wangapi
wanamjua Hamisi chilemba?.Huyu jamaa blangata yake imesimama vilivyo kwenye
soka.Hapa wachezaji kama uhuru selemani wataelewa ninachomaanisha.Uhuru selemani
chumvi nzuri inayopika mabao Simba ila kopo lake Chilemba lipo kawe linashona
viatu.Watu kama chilemba wana ujuzi mkubwa sana kwenye kukuza wachezaji
chipukizi ila hawajawezeshwa na hakuna anayewathamini.Mtu kama chilemba sio wa
kuwa mshona viatu.Angekua nchi za wenzetu chilemba angekua kwenye akademi ya
soka akienendelea kukitumia kipaji chake maridhawa kuzlisha vipaji vya vijana
chipukizi,Lakini kwetu Tanzania ataendelea kuwa mshona viatu huku wajanja
wajanja wachache wasio na ujuzi bali vyeti vingi wakiendelea kutafuna fursa
chache zilizopo.
Hawa wakina chilemba wapo wengi sana
nchini.Kuna watu kama Zagalo ni moja wa makocha waliowatoa wachezaji ligi kuu
lakini hakuna anayetambua mchango wake.Kuna mzee wa makamo mmoja anaitwa John Memba,wengi hupenda kumuita
‘coach memba’.Huyu mtu ana moyo wa dhati kujitolea kukuza soka la vijana,Mpaka
sasa ‘coach memba’ ameshafanikiwa kutoa wachezaji 11 ambao wapo kwenye academi
ya azam,wachezaji watano kwenye timu ya Ashanti na wachezaji 3 pan Afrika.Lakini mbaya zaidi amefanikiwa
kutoa wachezaji watano kwenda kwenye akademi ya Qatar,Tusishangae wachezaji hao
kuvaa uzi wa timu ya taifa ya Qatar wakiiwakilisha kwenye kombe la Dunia mwaka
2022.Huyu ndie John memba,sisi kwetu sio wa thamani ndio maana tumeamua
kumtumia john memba kama mlinzi katika shule ya Benjamin mkapa,ila waqatar siku
moja watarudi kumshukuru kwa mchango wake kwao.Wapo wengi wanaofanya hizi kazi
kwa mapenzi yao ya dhati,Nakumbuka nilishawai kumuuliza kiongozi mmoja wa simba
c ndugu akramu msangi al maarufu ‘aki mido’ ni jinsi gani ananufaika na timu
hiyo akaniambia kuwa “nafanya kazi bila malipo yoyote”.Ni mapenzi ya namna gani
haya.Huyu jamaa nae sifa yake kubwa ni kutafuta vipaji na kuvipeleka
kwenyeakademi za timu mbalimbali nchini ikiwemo azam na mtibwa sugar.Simba hawajali
wala kutambua mchango wake.Lakini Barcelona wanajua mchango wa Julio cosma
aliyekua anafanya kazi kama za aki mido.Hata timu kubwa kumbe hazijali makocha
wao wa chini?.
Ukiangalia makocha hawa hawahitaji pesa bali
wanahitaji kutoa walichonacho kichwani kwa maendeleo ya Soka letu.Hapa tff na
vilabu vyetu inabidi wawatengenezee
makocha hawa miundombinu ya kufanya kazi walizoitiwa Duniani.Muda ambao
chilemba anautumia kushona viatu angekua anautumia kwenye akademi ya soka
angekuwa ameshazalisha wakina uhuru selemani zaidi ya watano mpaka sasa.Muda
ambao mzee memba anautumia kulinda geti la shule ya Benjamin mkapa angekua ameshagundua vipaji vya vijana zaidi
ya hao aliyowagundua na kuwapeleka kwenye akademi mbali mbali za soka kupata
mafunzo zaidi .Chonde chonde kwa vilabu msiendelee kuyaacha makopo haya yakiwa
machafu jikoni,huku nyinyi mkiendelea kutumia chumvi walizozihifadhi kupikia
chakula kitamu mnachokula sasa.Pia tff inabidi
mtafute njia ya kuyahifadhi makopo haya kwa kujenga na kuendeleza
akademi za soka kwa maendeleo ya soka letu.
0 comments:
Post a Comment