728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, October 01, 2016

    EPL:EVERTON,PALACE HAKUNA MBABE ZATOKA SARE YA 1-1


    Liverpool,England.

    EVERTON imeshindwa kutamba nyumbani Goodison Park baada ya usiku huu kubanwa mbavu na kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Crystal Palace katika mchezo pekee wa ligi kuu England uliochezwa Ijumaa.




    Katikka mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Jon Moss na kushuhudiwa na watazamaji 38,758 ilishuhudiwa Romelu

    Lukaku akiiandikia Everton bao la kuongoza dakika ya 35 ya mchezo kwa mpira wa adhabu ya moja kwa moja.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.



    Kipindi cha pili ilikuwa ni Crystal Palace ndiyo waliotabasamu kwani dakika ya 50 Christian Benteke alifunga bao safi la kusawazisha kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Joel Ward na kufanya mchezo uishe kwa sare hiyo ya bao 1-1.

    Sare hiyo imeipandisha Everton mpaka nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi kuu baada ya kufikisha alama 14.Palace nayo imepanda mpaka nafasi ya 6 ikiwa na alama zake 11 baada ya kucheza michezo saba.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EPL:EVERTON,PALACE HAKUNA MBABE ZATOKA SARE YA 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top