Blida,Algeria.
TP Mazembe ya Congo DR imejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya jana Jumamosi Usiku kuibana Mouloundia Olympique de Bejai na kutoka nayo sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo mkali wa fainali ya kwanza uliochezwa katika uwanja wa Stade Mustapha Tchaker El Bouleïda jijini Blida,Algeria.
TP Mazembe ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 43 kupitia kwa Jonathan Bolingi aliyefunga kwa mkwaju wa penati.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili wenyeji Mouloundia Olympique de Bejai walijitutumua na kucheza soka la uhakika na kufanikiwa kusawazisha katika dakika ya 66 kupitia kwa nahodha wake Faouzi Yaya.
Timu hizo zitarudiana tena kwenye mchezo wa fainali ya pili utakaochezwa Jumapili ijayo Novemba 06 katika uwanja wa Stade du TP Mazembe huko Lubumbashi Congo DR.
Katika mchezo huo wa marudiano TP Mazembe inahitaji ushindi wowote ule au sare ya bila kufungana ili iweze kutwaa ubingwa. Mouloundia Olympique de Bejai wao wanahitaji ushindi wowote ule au sare ya kufungana mabao kuanzia mawili na kuendelea ili waweze kutwaa ubingwa huo.
Vikosi
MO Bejaia: Rahmani, Ferhat (Belkacemi 60),Rahal, Yaya, Khadir, Sidibe, Athmani Betorangal, Benmelouka, Salhi, Bouali.
TP Mazembe: Sylvain Gbohouo – Issama Mpeko, Salif Coulibaly, Roger Assale,Merveille Bope, Nathan Sinkala, Jona
0 comments:
Post a Comment