Sunderland, England.
MABAO mawili ya haraka haraka ya Mshambuliaji Olivier Giroud na mawili ya Winga Alexis Sanchez yameipa Arsenal ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Sunderland katika mchezo mkali wa ligi kuu England ulioisha hivi punde katika uwanja wa Stadium Light.
Alexis Sanchez alianza kuifungia Arsenal bao la kuongoza kwa kichwa katika kipindi cha kwanza akiunganisha krosi ya Alex Oxlade Chamberlain.Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili Sunderland walifanikiwa kusawazisha baada ya Jermaine Defoe kufunga kwa mkwaju wa penati.Bao hilo halikudumu sana kwani dakika chache baadae Olivier Giroud alifunga mabao mawili ya haraka haraka dakika chache baada ya kuingia akitokea benchi.Bao la nne limefungwa na Alexis Sanchez.
Ushindi huo umeifanya Arsenal ichupe mpaka kileleni baada ya kufikisha pointi 23 huku Sunderland wakiendelea kusota mkiani na pointi zao mbili.
0 comments:
Post a Comment