728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 21, 2016

    Evra:Luis Suarez ndiye namba 9 bora zaidi duniani


    Turin,Italia.

    BEKI wa kushoto wa Ufaransa,Patrice Evra, ametumia ukurasa wake wa instagram kuionyesha dunia kuwa hana kinyongo wala bifu lolote na adui wake wa muda mrefu Mruguayi Luis Suarez baada ya kutumia ukurasa huo kumpongeza mshambuliaji huyo kwa kutwaa zawadi ya kiatu cha dhahabu kufuatia msimu uliopita kuibuka mfungaji bora wa jumla wa Ulaya baada ya kupachika mabao 40.

    Evra,33,katika kipindi cha miaka mitano iliyopita amekuwa katika mahusiano mabovu na Suarez,29, lakini jana Alhamis alionyesha kuwa si mtu wa kuweka mambo moyoni baada ya kuandika ujumbe wa kumpongeza Suarez kwa kutwaa kiatu hicho cha dhahabu kwa mara ya pili mfululizo.




    Ameandika "Kwenye Instagram yangu ni upendo tu hakuna chuki.Luis!!Wewe ni mchezaji mzuri na namba tisa (9) bora zaidi duniani.Hongera.

    October 2011 Evra akiwa nahodha wa Manchester United alijikuta wakiingia katika bifu kali na Suarez aliyekuwa akiichezea Liverpool wakati huo baada ya Evra kumshtaki Suarez kuwa alimtolea lugha ya kibaguzi katika mchezo wao wa ligi kuu England.

    Hatua hiyo iliyofanya Suarez alimwe adhabu ya kutocheza michezo minane ya ligi kuu England pamoja na kutozwa faini ya Paundi 40,000.Adhabu hiyo ilipokwisha Suarez aligoma kumpa mkono Evra katika mchezo uliowakutanisha Februari 2012.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Evra:Luis Suarez ndiye namba 9 bora zaidi duniani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top