Manchester,England
Beki mahiri wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Ivory Coast ,Eric Bailly,atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili baada ya kuumia goti kwenye mchezo uliopigwa wikendi iliyopita dhidi ya Chelsea na kushuhudia Manchester United ikilala kwa mabao 4-0.
Bailly,22, amekuwa na msimu mzuri tangu ajiunge na klabu ya Manchester United akitokea kunako klabu ya manyambizi wa manjano Villarreal ya Hispania kwa kitita cha £30M!.
Chini ya Jose Mourinho bailly aliweza kuaminika Kutokana na aina yake ya uchezaji wa kutumia akili zaidi na kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma akishirikiana vyema na Mholanzi Daley Blind!..
Katika kipindi hicho chote Bailly atakosa jumla ya michezo 12 ambayo ni dhidi ya Manchester City- EFL, (H) Burnley - Epl(H),Fenerbahce - Europa league (A), Swansea-EpA (A) Arsenal-Epl(H), Feyenoord-Europa league (H), West ham-Epl(H), Everton-epl(A), Zorya-Europa league(A), Tottenham-Epl(H), Crystal Palace-Epl(A), West Bromwich Albion-Epl(A).
0 comments:
Post a Comment