728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, October 29, 2016

    EPL:Man United yabanwa nyumbani na Burnley,Man City yaua 4 ugenini.


    Manchester, England.

    MANCHESTER United imeshindwa kufurukuta nyumbani baada ya jioni ya leo kulazimishwa sare ya bila kufungana na Burnley katika mchezo mkali wa ligi kuu England uliochezwa katika uwanja wa Old Trafford ulioko jijini Manchester.

    Licha ya Manchester United kutawala mchezo kwa kiwango kikubwa lakini safu yake ya ushambuliaji ilishindwa kuupenya ukuta mgumu wa Burnley uliokuwa chini ya mlinzi Michael Keane na mlinda mlango Heaton.Ander Herrera wa Manchester United alionyeshwa kadi mbili za njana kwa mchezo mbaya.

    Katika mchezo mingine ya ligi hiyo Manchester City ikiwa ugenini imeichapa kwa mabao 4-0.Sergio Aguero amefunga mabao mawili na Ilkay Gundogan amefunga mawili.

    Middlesbrough imeichapa Bournemouth kwa mabao 2-0.Mabingwa Leceister City wametoka sare ya bao 1-1 na Tottenham.Bao la Leceister City limefungwa na Ahmed Mussa huku Vincent Janssen akifunga kwa upande wa Tottenham.

    Watford ikiwa nyumbani Vicarage Road imeichapa Hull City kwa bao 1-0.Shukrani kwa bao la kujifunga la Dawson.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EPL:Man United yabanwa nyumbani na Burnley,Man City yaua 4 ugenini. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top