Dar Es Salaam,Tanzania.
VINARA wa ligi kuu bara Simba SC hatimaye wamefanikiwa kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Kimataifa wa Congo DR,Mussa Ndusha,baada ya Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa ( ITC) kupatikana.
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC Godfrey Nyange Kaburu amethibitisha kupatikana kwa ITC hiyo na kuongeza kuwa tayari imeshafika Dar Es Salaam.
Hii ina maana kwamba Simba SC sasa itaweza kumtumia Ndusha kwenye michezo yake ya ligi Kuu bara pamoja na michuano ya kombe la FA maarufu kama Azam Confederation Cup.
Hadi sasa, Ndusha ameichezea Simba SC mechi mbili za kirafiki ikishinda 4-0 dhidi ya AFC Leopard na katika sare ya 1-1 na URA ya Uganda, zote Uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam.
0 comments:
Post a Comment