Riio Grande do Norte,Brazil.
BRAZIL ikicheza katika dimba lake la nyumbani la Arena das Dunas imeichapa Bolivia kwa mabao 5-0 katika muendelezo wa michezo ya kanda ya Amerika Kusini (CONMEBOL) ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 litakalofanyika nchini Urusi.
Katika mchezo huo ilishuhudiwa Neymar Jr akiibuka nyota wa mchezo baada ya kufunga bao moja na kutengeneza mengine mawili na kuifanya Brazil iwe imecheza michezo mitatu na kushinda yote.
Neymar Jr alianza kuifungia Brazil bao la kuongoza dakika ya 11 ya mchezo kabla ya kutengeneza mabao mengine mawili yaliyofungwa na Filipe Luís dakika ya39 pamoja na Gabriel Jesus dakika ya 43.Mabao mengine ya Brazil yamefungwa na Philippe Coutinho dakika ya 25 na Roberto Firmino dakika ya 75.
Neymar Jr afikisha mabao 300
Bao moja alilofunga dhidi ya Bolivia limemfanya Neymar kufikia mabao 300 katika ngazi ya klabu na timu ya taifa.Bao lake la 49 akiwa na Brazil.Nyuma ya Pelé mwenye mabao 95, Ronaldo 67', Zico 66'na Romário 56'.
Katika mchezo mwingine Ecuador ikiwa nyumbani Santiago imeichapa Chile kwa mabao 3-0.Shukrani kwa mabao ya Antonio Valencia,Cristian Ramirez na Felipe Caicedo.
Uruguay ikiwa nyumbani Monteivideo imechomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Venezuela kwa mabao ya Edinson Cavani aliyefunga mara mbili pamoja na Nicolas Lodeiro.
0 comments:
Post a Comment