Cardiff,Wales.
KLABU ya Cardiff City inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini England imekiongezea nguvu kikosi chake baada ya jioni ya leo kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Crystal Palace,Marouane Chamakh,kwa mkataba wa miezi mitatu akiwa kama mchezaji huru.
Cardiff City maarufu kama
Bluebirds imemsajili Chamakh mwenye umri wa miaka 32 sasa ili kuiongezea makali safu yake ya ushambuliaji ambayo katika siku za hivi karibuni imekuwa haifanyi vizuri sana.
Akiongea baada ya kukamilika kwa usajili huo kocha mpya wa Cardiff City,Neil Warnock,amesema ameamua kumsajili Chamakh kwa kuwa ni mchezaji mzuri na pia ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani.Pia anamjua vyema kwani aliwahi kufanya nae kazi katika klabu ya Crystal Palace.
Mbali ya Chamakh,Cardiff City,pia imemsajili beki wa zamani wa Leeds
United Muivory Coast,Sol Bamba,kwa mkataba utakaodumu mpaka katika majira ya joto ya mwaka 2018.
0 comments:
Post a Comment