Mouscron,Ubelgiji.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania,Mbwana Ally Samatta,leo usiku mishale ya saa 3:30 atakuwa na kibarua kigumu cha kuiongoza KRC Genk, ugenini huko Stade Le Canonnier kuvaana na Royal Excel Mouscron katika mchezo wa mzunguko wa kumi wa ligi kuu ya Ubelgiji maarufu kama Belgian Pro League
KRC Genk inaingia katika mchezo wa leo ikiwa katika nafasi ya tisa baada ya kujikusanyia pointi 13 kufuatia kucheza michezo tisa.Royal Excel Mouscron iko nafasi ya kumi na mbili baada ya kujikusanyia pointi 9 katika michezo tisa.
Michezo Mingine - Belgian Pro League
KV Kortrijk v Standard Liege
Sint Truidense VV v KVC Westerlo
Waasland Beveren v KAS Eupen
Mouscron-Peruwelz v KRC Genk
0 comments:
Post a Comment