Genk,Ubelgiji.
KLABU ya KRC Genk inayochezewa na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania,Mbwana Ally Samatta,imefanikiwa kushika uongozi wa kundi F baada ya Alhamis Usiku kuichapa Athletic Bilbao ya Hispania mabao 2-0 katika mchezo mkali wa michuano ya Euro Ligi uliochezwa katika uwanja wa Cristal Arena huko jijini Genk,Ubelgiji.
Iliwachukua KRC Genk dakika 40 tu za kipindi cha kwanza kuchukua uongozi katika mchezo huo baada ya Jakub Brabec kufunga bao la kuongoza lililodumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili walikuwa ni KRC Genk tena walioendelea kutabasamu baada ya mlinzi wake wa kimataifa wa Nigeria Wilfred Ndidi kufunga bao la pili katika dakika ya 83 ya mchezo.Samatta aliingia katika dakika ya 53 kuchukua nafasi ya Thomas Buffel.
Ushindi huo umeipeleka KRC Genk mpaka kileleni mwa kundi F baada ya kujikusanyia pointi sita katika michezo mitatu.
Kundi F
1. KRC Genk, 6p
2. Rapid Wien, 4p
3. Sassuolo, 4p
4. Athletic Bilbao, 3p
0 comments:
Post a Comment