Toulouse,Ufaransa.
ARSENAL imeanza mapema maandalizi ya kujiandaa na maisha bila ya kipa wake mkongwe,Petr Cech kwa kutuma maskauti wake kwenda nchini Ufaransa kumfuatilia kipa kijana wa Toulouse,Alban Lafont.
Kwa mujibu wa habari kutoka katika gazeti la michezo la Ufaransa la L’Equipe,Arsenal wamevutiwa na maendeleo ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 17 na wako tayari kumfanya kuwa mrithi wa muda mrefu wa Cech mwenye umri wa miaka 34 na ambaye amebakiza miezi 18 kumaliza mkataba wake.
Mbali ya Arsenal vilabu vya Watford, Juventus na Porto navyo vimeripotiwa kuwa katika mbio za kumuwania kipa huyo ambaye msimu huu tayari ameichezea Toulouse michezo tisa.Akifanikiwa kucheza michezo mitatu bila ya kuruhusu bao lolote kugusa wavu wake.
Msimu uliopita Lafont aligonga vichwa vya habari za michezo nchini Ufaransa baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kucheza ligi ya juu ya nchi hiyo [Ligue 1] pale alipokichezea kikosi cha kwanza cha Toulouse akiwa na umri wa miaka 16 na siku 310.Kwa sasa ana mkataba na Toulouse mpaka mwaka 2020.
0 comments:
Post a Comment