London,England.
DROO ya michuano ya kombe la ligi maarufu kama EFL imefanyika jana Jumatano Usiku muda mfupi baada ya kumalizika kwa michezo ya hatua ya 16 bora.
Manchester United ambayo imetinga robo fainali kwa kuwabanjua wapinzani wao Manchester City kwa bao 1-0 itakutana na Westham United ambayo imeingia hatua hiyo kwa kuifunga Chelsea kwa mabao 2-1.
Arsenal itakuwa Nyumbani Emirates kuvaana na Southampton wakati Leeds United wakisafiri mpaka Anfield kupepetana na Liverpool.Hull City watakuwa nyumbani KC Stadium kucheza na Newcastle United.
Droo Kamili
Liverpool v Leeds United
Manchester United v West Ham United
Hull City v Newcastle United
Arsenal v Southampton
Michezo yote ya robo fainali itachezwa kati ya Novemba 28/29
0 comments:
Post a Comment