728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, October 25, 2016

    Nahodha wa zamani wa Brazil afariki duniani


    Rio de Janeiro,Brazil.

    NAHODHA na beki wa zamani wa kulia wa Brazil,Carlos Alberto,amefariki dunia leo mchana kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 72.

    Alberto aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Brazil kilichotwaa kombe la dunia lililofanyika mwaka 1970 nchini Mexico huku yeye akifunga bao moja katika ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Italia amekumbwa na umauti huo nyumbani kwake Rio de Janeiro.

    Mpaka umauti unamfika ,Alberto alifanikiwa kuichezea Brazil jumla ya michezo 53.Pia alivichezea vilabu vya Fluminense and Santos zaidi ya michezo 400 na kufanikiwa kuvibebesha mataji mbalimbali ya ndani.

    Aidha Alberto aliyewahi kuwa kocha wa zamani wa vilabu vya Flamengo na Botafogo vyote vya Brazil,anatajwa kuwa ni mmoja kati ya mabeki bora zaidi wa kulia kuwahi kutokea duniani huku bao alilofunga katika mchezo wa finali ya kombe la dunia la mwaka 1970 dhidi ya Italia likitajwa kuwa ni moja kati ya mabao bora zaidi kuwahi kufungwa katika historia ya michuano hiyo kwani kabla ya bao hilo mpira uliguswa na wachezaji tisa wa Brazil.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nahodha wa zamani wa Brazil afariki duniani Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top