728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, October 25, 2016

    Yanga yaajiri Mzungu kuweka sawa hesabu za klabu.


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    YANGA SC imemuajiri Mfaransa,Jerome Dufourg kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo kwa Mkataba wa miaka mitatu.

    Dufourg aliyewahi kufanya kazi Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) kama mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam wakati wowote kuanza kazi.

    Dufourg mwenye umri wa miaka 30 atakuwa Dar es Salaam mwezi ujao na ataanza kazi rasmi Novemba 19 baada ya kumalizana na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji.

    Jukumu la kwanza kubwa la Dufourg na kuhakikisha mapato ya klabu yanazidi matumizi. Mwaka jana Yanga iliingiza Sh Bilioni 1.3 wakati ilitumia Sh Bilioni 2.8.

    Tayari Yanga imebadilisha benchi la Ufundi,ikimuondoa aliyekuwa kocha mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm na kumuajiri Mzambia, George Lwandamina.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga yaajiri Mzungu kuweka sawa hesabu za klabu. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top