Amsterdam,Uholanzi.
PAUL Pogba (Pichani) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Ufaransa bao la umbali wa mita 30 na kuiwezesha kuchomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uholanzi katika mchezo mkali wa kundi A wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi huko Amsterdam Arena,Uholanzi.
Katika mchezo mwingine wa kufuzu kombe la dunia,mabingwa wa Ulaya,Ureno,wameichapa timu kibonde ya Visiwa vya Faroe kwa mabao 6-0 huko Torsvoellur Stadium.
Ureno imepata mabao yake kupitia kwa André Silva aliyefunga mara tatu,Cristiano Ronaldo,João Moutinho na João Cancelo wamefunga mara moja moja.
MATOKEO MENGINE
GROUP A
Belarus 1-1 Luxembourg
Sweden 3-0 Bulgaria
GROUP B
Andorra 1-2 Switzerland
Faroe Islands 0-6 Portugal
Latvia 0-2 Hungary
GROUP H
Bosnia-Herzegovina 2-0 Cyprus
Estonia 0-2 Greece
Gibraltar 0-6 Belgium
0 comments:
Post a Comment