Dar Es Salaam,Tanzania.
AFRICAN Lyon imeutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Uhuru maarufu kama Shamba la Bibi baada ya mchana wa leo kuichapa Mbeya City kwa jumla ya mabao 2-0.
Mabao yote yamepatikana kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Tito Okello alianza kuifungia bao la kuongoza African Lyon katika dakika ya 55 kwa mkwaju mkali wa karibu kabla ya Rehani Kibingu kufunga bao la pili katika dakika ya 95 akiunganisha pasi ya Hood Mayanja.
Ushindi huo unaifanya African Lyon ifikishe pointi 13 na kuchupa mpaka nafasi ya 11.Mbeya City imebaki katika nafasi ya 10 na pointi zake 13.
0 comments:
Post a Comment