728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, October 08, 2016

    KOMBE LA DUNIA:ENGLAND YATAMBA NYUMBANI YAICHAPA MALTA 2-0 WEMBLEY

    London,England.

    MABAO mawili ya kipindi cha kwanza yameipa England ushindi safi wa mabao 2-0 dhidi ya Malta katika mchezo mkali wa kundi F wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia ulioisha hivi punde katika uwanja wa Wembley,London.

    Daniel Sturridge alianza kuifungia England bao la kuongoza kwa kichwa katika dakika ya 29 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Jordan Henderson.Bao la pili limefungwa dakika ya 38 na Dele Alli baada ya kutokea piga nikupige langoni kwa Malta.

    Ushindi huo umekuwa mwanzo mzuri kwa Kocha wa muda wa England,Gareth Southgate, aliyeanza kukinoa kikosi hicho siku 11 zilizopita akichukua nafasi ya Sam Allardyce aliyejiuzulu.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOMBE LA DUNIA:ENGLAND YATAMBA NYUMBANI YAICHAPA MALTA 2-0 WEMBLEY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top