728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, October 07, 2016

    TFF HAINA TAARIFA ZA UKODISHWAJI WA YANGA

    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema linasubiri barua rasmi ya ukodishwaji wa Yanga ndipo itoe tamko. Baraza la Wadhamini wa Yanga juzi liliridhia na kumkodisha rasmi timu Mwenyekiti Yusuf Manji kwa miaka kumi.

    Kwa mujibu wa taarifa ya Yanga jana,Baraza la Wadhamini ambao kwenye mkataba huo linajulikana kama (mmiliki) limeingia mkataba na Kampuni ya Yanga Yetu Limited (mkodishaji) kama maazimio ya mkutano wa dharura wa wanachama wa klabu hiyo Agosti 6 mwaka huu.

    Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa alisema hawajapata bado taarifa rasmi na kwamba watatolea maamuzi watakapopata taarifa hizo.

    Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdetit alithibitisha kuwa baraza hilo la wadhamini chini ya Fatuma Karume limemkabidhi rasmi Manji timu ili ijipange ndani ya miaka 10 timu itakaporejeshwa ijiendeshe yenyewe bila kutegemea wafadhili.

    Katika mkutano wa dharura wa klabu hiyo Manji aliomba apewe klabu kwa miaka 10 na katika kipindi hicho atakuwa anachukua asilimia 75 ya mapato ya timu, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.Na katika kipindi hicho cha miaka 10, timu ya soka na nembo ya klabu zote zitakuwa chini yake Manji.

    Aidha, Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu,Francis Kifukwe alisema baada ya wanachama kuridhia mpango huo, wao wanampa pia ridhaa hiyo Manji.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TFF HAINA TAARIFA ZA UKODISHWAJI WA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top